Michezo

Baba Mzazi wa Kichuya amgomea mwanae kusaini Simba, asubiri ofa ya TP Mazembe

Baba mzazi wa kiungo wa Simba, Shiza Ramadhani Kichuya mzee Ramadhani Kichuya amemshauri mwanae huyo kutosaini mkataba mpya na klabu hiyo na badala yake asubiri ofa kutoka Tp Mazembe ya Congo DR.

Kiungo wa Simba, Shiza Ramadhani Kichuya

Mzee Ramadhani Kichuya amemuonya mwanae kutokuanguka saini tena kwa mabingwa hao wapya wa ligi kuu ya Vodacom Tanzania Bara na badala yake kutimkia Mazembe akidai kuwa mashabiki wa wanamsimbazi wameshindwa kumpa thamani anayostahili.

TP Mazembe yamfukuzia Kichuya ” La Pulga” kimya kimya

Shiza Kichuya anatarajia kumaliza mkataba wake ndani ya Simba mwezi Juni mwaka huu wakati ligi kuu ikiwa inaelekea ukingoni.

Kiungo huyo mshambuliaji wa amejiunga na Simba akitokea kwa mabingwa wazamani wa ligi klabu ya Mtibwa Sugar akiwa na wachezaji wenzake Mzamiru Yassin na Mohammed Ibrahim.

Wakati baba mzazi wa Kichuya amesema kuwa anahitaji kuona mwanae anapata mafanikio kupitia mpira na hivyo muda umefika sasa kwa mwanae kucheza soka la kulipwa kwenye klabu kubwa kama TP Mazembe ambayo alipata kuitumikia Samatta.

Kichuya amehusishwa na kuhitajika na TP Mazembe baada ya kufanya vizuri kwenye mchezo wa kirafiki baina ya timu ya taifa ya Tanzania (Taifa Stars) dhidi ya DR Congo.

 

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents