Jiunge ufaidi miezi 2 bure!

Baba mzazi wa Meghan Markle kutohudhuria kwenye harusi ya mwanae

Huenda Baba Mzazi wa Meghan Markle, Thomas Markle asihudhurie kwenye harusi ya mtoto wake huyo na mjukuu wa malkia wa Uingereza Prince Harry inayotarajiwa kufanyika Mei 19 ya mwaka huu.


                                   Baba mzazi wa Meghan Markle, Thomas Markle

Kwa mujibu wa taarifa hiyo iliyotolewa na Kasri ya Kensington ambapo ni makazi ya Prince Harry, imeeleza sababu ya kutohudhuria ni kutokana na kuwa na shinikizo la damu.

“This is a deeply personal moment for Ms Markle in the days before her wedding. She and Prince Harry ask again for understanding and respect to be extended to Mr Markle in this difficult situation,” imesema taarifa hiyo ya Ikulu ya Kensington.

Hata hivyo taarifa zilizozagaa ni kuwa mzee Markle hatohudhuria kwenye sherehe hiyo kutokana na tuhuma za kupigwa picha kwa makubaliano ya siri, hivyo ana hofia kumuaibisha binti yake.

Related Articles

Bongo5

FREE
VIEW