Habari

Baba mzazi wa Pancho Latino afunguka juu ya kifo cha mwanae ‘niliongea nae juzi, lazima azikwe huku kijijini’ (+Audio)

Baba Mzazi wa muandaaji wa muziki nchini Tanzania, Marehemu Pancho Latino amesema kuwa mtoto wake atazikwa kijijini kwao Msingisi Wilani Gairo mkoani Morogoro.

Mchungaji Simon Magawa amesema kuwa kwa mara ya kwanza alizipata taarifa za kifo cha mtoto wake kupitia mitandao ya kijamii na baadae akampigia kaka wa marehemu ambaye alikuwa anaishi naye hapa Dar es salaam.

Kuhusu ratiba ya mazishi Mchungaji Magawa amesema kuwa mtoto wake atazikwa kijijini hapo siku ya Jumamosi endapo ratiba itaenda kama ilivyopangwa.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents