Habari

Baba mzazi wa Rais Museveni wa Uganda afariki dunia

Mzee Amos Kaguta ambaye ni baba mzazi wa Rais Yoweri Museveni wa Uganda amefariki dunia leo asubuhi huko jijini Kampala, Uganda.
Amos-Kaguta
Mzee Amos Kaguta amefariki akiwa na umri wa miaka 96 na inasemekena alikuwa anasumbuliwa na maradhi ya tumbo na a kichwa ambapo alikuwa amelazwa katika hospitali ya IHK (International Hospital Kampala).

Rais Museveni ndio mtoto wa kwanza wa Mzee huyo aliyezaliwa na mke wake wa kwanza marehemu Esteri Kokundeka Nganzi.

Mzee Kaguta alikuwa akijulikana kwa ufugaji wake wa ng’ombe. Mipango ya mazishi inaendelea.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents