Burudani

Baba wa Ali Kiba kuzikwa katika makaburi ya Kisutu jijini Dar

Mwanamuziki Ali Kiba amefiwa na baba yake Saleh Kiba leo katika Hospitali ya Muhimbili alipokuwa amelazwa kwa takribani siku 21.

Akithibisha taarifa ya kifo hicho, Abdu Kiba ambaye ni mdogo wa Ali Kiba alisema ni kweli baba yao amefariki na msiba upo nyumbani kwao Kariakoo Mtaa wa Muheza.

Kwa mujibi wa taarifa za kutoka ndani ya familia hiyo, mazishi yatafanyika Alhamisi hii saa 10 jioni katika makaburi ya Kisutu jijini Dar es salaam.

Ofisa Uhusiano wa Hospitali ya Taifa ya Muhimbili (MNH), Neema Mwangomo amesema Mzee Saleh, alifikwa na mauti leo saa 12:05 katika hospitali hiyo.

Neema alibainisha kwamba baba huyo alifikishwa hospitalini hapo tangu Desemba 27 mwaka jana.

Source: Mwanaspoti

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents