Burudani

Baba wa Maundo Zoro awajia juu Shilawadu

Baba mzazi wa mwanamuziki Maunda Zoro na Banana Zorro, mzee Zahir Zorro amewajibu wanoandika habari kuwa binti yake  amekongoroka.

Kupitia mtandao wa Instagram, mzee huyo ambaye pia ni mwanamuziki amewawakia watu wanaopakaza kuwa binti yake  amekongoroka kutokana na matumizi ya  pombe haramu ya Gongo pamoja na madawa ya kulevya aina ya Bangi.

Aisee, huyu ndie Maunda Zorro wangu Shillawadu wanadai amekongoloka na Gongo na Bangi. Ajabu Waajiriwa wa Media ya Sifa Wanaandika bila ku- Balance Khadithi. Walienda Muhoji Hawa niliye mlea kwangu kama Binti yangu zaidi ya Miaka miwili. Akaondoka, Akarudi baadae Akaondoka tena bila kufukuzwa. Leo anajaribu kuukata Mkono uliomlisha kwa Wembe. Waniombe Radhi!

Shilawadu wanapaswa kufahamu hili, umaweza Wadanganya Watu wote muda au kipindi Fulani tu. Hutoweza kuwadanganya Watu Muda au Kipindi chote. Nawaambia kwa hili Wamechemsha!

Mama yake na msanii Hawa wa Nitarejea alinukuliwa akisema katika kipindi cha Shilawadu kuwa Maunda Zoro na binti yake ni marafiki na huwa wanavuta bangi na kunywa gongo nyumbani kwake.

Na Laila Sued

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents