Baba yake na Beyonce agusia uwezekano wa ziara na album mpya ya Destiny’s Child
Ikiwa ni takriban miaka 10 tangu itoke album mpya ya Destiny’s Child, baba yake na Beyonce, Mathew Knowles amesema huenda kundi hilo likaungana kwa mara nyingine.
Akiongea na mtandao wa The Huffington Post, Knowles ambaye bado anasimamia kazi za kundi hilo alisema mashabiki watarajie kitu.
“Nina matumaini makubwa kuwa wasichana hawa watarejea na album na ziara. Ninafanyia kazi miradi michache ya Destiny’s Child kwa sasa,” alisema.
“Kitabu changu cha pili kitakuwa ni historia ya Destiny’s Child. Ninaongea na watu wa filamu na TV kwa sasa, kuhusiana na filamu ya Destiny’s Child au series, kitu kama hicho. Lakini bado nawasimamia wasichana hawa, na nina matumaini miaka miwili au mitatu ijayo tutaona makubwa kutoka kwao.”
Knowles amewahi pia kuwa meneja wa Beyonce.