Tragedy

Dully Sykes ataja sababu ya kifo cha baba yake, mastaa wamlilia Mzee Ebby Sykes

Vidonda kwenye miguu vilivyosambaza sumu hadi kwenye mwili wake, ndio chanzo cha kifo cha mwanamuziki mkongwe nchini, Ebby Sykes, kwa mujibu wa mwanae, Dully Skyes. Mzee Sykes amefariki dunia akiwa na umri wa miaka 62. Angetimiza miaka 63 February 24.

10958102_336497629887424_191661160_n

Dully ameimbia blog ya millardayo.com kuwa kwa miezi kadhaa baba yake alikuwa akisumbuliwa na vidonda hivyo ambavyo vilishindwa kupona kwa sababu alikuwa akivuta sigara.

“Vidonda vilishindwa kupona kwaajili ya moshi,” alisema Dully. “Lakini alikuwa hana tatizo lolote, baba yangu mimi mtu mmoja strong. “Miezi miwili alikuwa anavumilia tu lakini miezi mingine ya mwisho ile ndio ikawa serious sasa,” aliongeza.

Dully anadai kuwa kipindi baba yake anaugua aliamua kumchukua na kuishi naye kwake kwa wiki mbili kabla ya kwenda kuishi tena kwa dada yake (shangazi yake Dully) ambako alipelewa kwenye hospitali ya Muhimbili alikofikwa na mauti.

Mazishi yanafanyika Jumatatu hii kwenye makaburi ya Kisutu.
Mastaa mbalimbali wametuma salamu zao za rambirambi kufuatia msiba huo. Chini ni baadhi ya salamu hizo.

Q-Chief
Siku zote amekuwa karibu yetu na kuwa mzazi wa wote alipenda usawa bila kujali sisi nani msiba huu umenigusa saaana kwani hata mwanangu kipenzi wakike ni rafiki yake kipenzi najua nitashindwa kujizuia pale atakaponiuliza baba abuu yule babu wa guiter yuko wapi sijui kama nitakuwa tayari kuipokea hali hii sina mengi uncle abby mungu rabbi akufanyie wepesi katika safari yako ndefu msiba hauzoeleki na hisia hazielezeki longlife papa forever young will alwayz carry ur spirit rip uncle abby we miss u…. RIP pole sana DULLY

Linex
Nachukua nafasi hii kuipa pole family ya mwanamuziki mwenzangu @princedullysykes kwa kumpoteza baba yake mpendwa mzee Sykes Yeye alie mleta na hatimae amemtwaa R.I.P baba wa kila mtu Mungu akupumzishe kwa amani na awape nguvu ndugu jamaa na marafiki katika kipindi hichi kigumu

Shaa
Pole sana kaka Dully na Familia nzima ya Mzee Sykes…Mwenyezi Mungu awape nguvu katika kipindi hiki kigumu na kuilaza roho ya marehemu mahali pema peponi..Amen.

Shamsa Ford
shamsaford May God rest his soul in peace..pole sana kaka yangu,rafiki yangu dully tupo pamoja katika kumuombea marehemu.@princedullysykes

TID
na lilahi…….RIP my father,my mentor #AbbYSyKeS am gon miss ur guitar kama umepiga hivi @princedullysykes

Izzo Bizness
MUNGU akupumzishe kwa amani mzee wetu baba yetu mzee sykes pole sana kaka Dully kwa kipindi hiki kigumu

Mr Blue
R.i.p baba yetu tulikupenda sana mungu amekupenda zaidi..dah..inaniuma sana kuondokewa na mzee wangu…

Alikiba
Pole sana @princedullysykes kwa kufiwa na Baba yako mzazi. Inna Lillahi Waina Illahy Rajoun. #RIP

Joh Makini
Pole sana chalii aangu @princedullysykes mzee katutangulia Bwana alitoa na bwana ametwaa na ampumzishe Baba yetu mahala pema peponi….amen

Jux
R.I.P mzee wetu pole sana bro @princedullysykes na familia yako yote

Shilole
R.IP mzee wetu baba yake na @princedullysykes Upumzike salam njia yetu ni moja

Mzee Sykes alizaliwa tarehe 24 February, 1952. ‎Mungu ailaze roho yake mahali pema.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents