Tia Kitu. Pata Vituuz!

Baba yake Samatta aeleza “Nililia baada ya mwanangu kufunga goli dhidi ya Man City kwenye fainali, Sikuamini kama ni yule niliyemzaa mimi” – Video

Baba yake Samatta aeleza "Nililia baada ya mwanangu kufunga goli dhidi ya Man City kwenye fainali, Sikuamini kama ni yule niliyemzaa mimi" - Video

Katika mahojiano aliyofanya na Mtangazaji wa BBC @salim_kikeke baba mzazi wa kapteni wa timu ya taifa Stars pia mshambuliaji wa klabu ya Aston Villa @samagoal77 ameeleza jinsi alivyokuwa anajisikia baada ya Samatta kufunga goli katika mchezo wa fainali ya Carabao cup dhidi ya Manchester City.

Ikumbukwe Samatta ameweka rekodi ya kuwa Mtanzania wa kwanza kucheza katika uwanja wa Wembley pia kufunga goli katika uwanja huo lakini pia kufunga goli katika mchezo wa fainali.

Mbali na hilo Samatta ameingia kwenye rekodi ya kuwa mchezaji wa pili kumfunga Pep Guardiola kwenye mchezo wa fainali baada ya Wayne Rooney kufunga mwaka 2011 katika mchezo wa fainali baina ya Manchester United dhidi ya Barcelona kwenye fainali za UEFA ambapo United walifungwa goli 3-1.

Ujumbe wa Samatta ni huu akiwa na baba yake mzee Ally Samatta.

Baba Samatta ameongea mengi sana msikilize kwa makini.

By Ally JUma.

 

Related Articles

Back to top button
Close
Bongo5

FREE
VIEW