BurudaniVideos

Baba yangu aliathirika na madawa ya kulevya – Hemedy PHD

Janga la matumizi ya madawa ya kulevya hapa nchini lina madhara makubwa katika familia nyingi hata katika zile ulikuwa hutarajii.

Muimbaji wa R&B, Hemedy PHD amedai kuwa baba yake mzazi ni mmoja wa watu walioathirika na madawa ya kulevya.

“Baba yangu aliathirika na madawa ya kulevya. Tulijaribu kumtibu zaidi ya mara 6 ikashindikana,” Hemedy aliiambia Millarday.com.

“Mwisho wa siku tukagundua kwamba nia inatoka moyoni, ni kwako mwenyewe binafsi unaamua kwamba mimi hiki kitu hapana, naacha,” ameongeza.

Kwenye mahojiano hayo pia Hemedy alikanusha tetesi kuwa naye ni mtumiaji wa unga.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents