Burudani

Babu Tale alia na ugumu wa ajira

By  | 

Meneja wa Diamond Platnumz na mmiliki wa kundi la Tip Top Connection,Babu Tale ameguswa na hali ya ugumu wa ajira kwa sasa hususani kwa wasomi wengi waliomaliza vyuo akiwemo mke wake.

Tokeo la picha la Babu tale

Babu Tale

Babu Tale amesema licha ya Connections zote alizonazo lakini bado mke wake aliyemuita msomi wake anasota kutafuta ajira .

Msomi wangu bado yupo nyumbani na degree yake ipo kabatini nakumbuka nilisema ajira kamlete ila kwake imekua ngumu pamoja na connection zote nilizo nazo bado mtiani“,Ameandika Babu Tale kwenye ukurasa wake wa Instagram.

Babu Tale ameenda mbali zaidi kwa kuangalia Ajira za Serikalini ambapo amegusia zile taarifa zilizosambaa mtandaoni kuwa Serikali haitaajiri watu wenye umri wa kuanzia miaka 30 na kusema kuwa kwa mpango huo hela yake aliyotumia kumsomesha mke wake imeenda bure kabisa

“na hivi serikali imetangaza juu ya miaka 30 ajira hakuna pesa yangu imeenda bure IFM”ameandika Babu Tale.

By Godfrey Mgallah

 

Jiunge na Bongo5.com sasa

Usipitwe!! Jiunge nasi kupitia Facebook, Twitter na Instagram ili kupata habari zote za town! Usikose kujiunga na Youtube kuangalia video zote kali kutoka Bongo5!

Add a comment

comments