Burudani ya Michezo Live

Babu Tale ashauriwa kutorudi nyuma ndoto ya Ubunge kumuenzi mke wake, Shammy

Wiki iliyopita ilikuwa ngumu sana kwa meneja wa WCB, Babu Tale ambaye alifiwa na mama watoto wake watatu ikiwa ni mwezi mmoja toka tetesi za kugombea Ubunge zizagae kwa kasi kwenye mitandao ya kijamii.

Katika shughuli za mazishi ya mke wake, Mkuyuni Morogoro wengi ambao walipata fursa ya kuongea kama nafasi kumpatia pole, wengi walionesha kumtia moyo huku wengine wakimtaka kuendelea na harakazi zake za kutaka kugombea Ubunge ili kuwakomboa wananchi wa eneo hiyo ambalo lilionekana kuwa nyuma kimaendeleo.

Mkubwa Fella ambaye ni mmoja kati ya mtu wa karibu wa Tale kwenye kazi na maisha, amemtaka Tale kutorudi nyuma katika ndoto ambayo alikuwa nayo.

“Changamoto ni sehemu moja katika maisha yetu wanadamu hivyo kwa changamoto na mitihani unayopitia isikufanye ukate Tamaa, isikufanye urudi nyuma sisi tunaimani na wewe na tunaamini unaweza kwasababu sifa zote za uongozi unazo.,” aliandika Mkubwa Fella kupitia Instagram yake.

Aliongeza, “Kwa Kipindi Chote Tumefahamiana Umekuwa Dereva Mzuri Kwetu Na Kwa Jamii Pia Na Hili Liko Wazi. Ni Muda Sasa Wa Kuwatumikia Wananchi Wa Mkoani Kwako Morogoro Vijijini. Ushatia Nia Ya Kugombea Ubunge Morogoro Vijijini Hivyo Changamoto Na Mitihani Uliyonayo Isikufanye Urudi Nyuma Inuka Pangusa Vumbi Anza Safari Nasi Tuko Nyuma Yako Bega Kwa Bega Kuhakikisha Lengo Lako Linafanikiwa @Babutale Mbunge Mtarajiwa Morogoro Vijijini #Gotale #Nendatale #Hapakazitu #TanzaniaYaSasa cc @ikulu_mawasiliano @ccmtanzania,”

Naye Sallam ambaye ni meneja wa WCB, alisema baada ya mazishi ya mke wa Tale watarejea Mkuyuni kwaajili ya kuchonga barabara ambayo siku ya tukio ilionekana kuwa kero kutokana kuwa na mashimo mengi hivyo na kuwa kero kwa wageni.

Related Articles

Back to top button
Close
Bongo5

FREE
VIEW