Burudani

Baby Madaha adai kuingia mkataba wa milioni 200 na Steps kusambaza filamu yake

Msanii wa filamu Bady Madaha aliye chini ya kampuni ya Candy n Candy amedai kuingia mkataba wa shilingi milioni 200 na kampuni ya usambazaji filamu nchini, Steps Entertainment ili kusambaza filamu yake mpya ‘The Gal Bladder’ Afrika Mashariki na kati.

http://www.youtube.com/watch?v=_tlU9Qfm8oE

Akizungumza na Bongo5 leo, Baby Madaha amesema baada ya kufanya kazi ya uzinduzi wa filamu hiyo sasa kazi ya usambazaji wanaikabidhi kampuni ya Steps.

“Kampuni ambayo inanisimamia Candy n Candy baada ya kumaliza kazi ya kuzalisha filamu ya ‘The Gal Bladder’ kilicho baki ni kutafuta nani atasambaza kazi hii AfriKa mashariki na kati,tukaona tuingine mkataba na Steps kwa milioni 200,” amesema.

Pia Baby Madaha amesema anajiandaa kuanza kushoot filamu nyingine itakayofanyikia Afrika Kusini huku akiwa amewashirikisha baadhi ya wasanii wa Afrika Mashariki na Kati.

“Mwaka huu kuna mambo mengi yanakuja kutoka kwa Baby Madaha kuanzia kwenye muziki na filamu,ila ambacho kipo mbioni ni filamu ambayo nitaanza kushoot Afrika Kusini.”

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents