Bongo Movie

Baby Madaha, Madee, Tunda Man na Chidi Benz kuipa tafu ‘Bongo Dar es Salaam’ ya Dude

Ile show iliyokuwa maarufu kwenye kituo cha runinga cha TBC1, ‘Bongo Dar es Salaam’ inatarajia kurejea kwa kishindo kwenye screen.

Staa wa show hiyo Kulwa Kikumba maarufu kama Dude amezungumza kuhusu kuanza tena kwa show hiyo ambayo ipo kwenye hatua ya kurekodiwa.

“Tunarekodi michezo mingi zaidi ili tukianza kuirusha hatupumziki,” anasema Dude.

Amesema ili kuufanya ujio wa show hiyo kuwa wa kishindo zaidi ameamua kuwashirikisha mastaa wa muziki nchini wakiwemo Bahati Bukuku ,Madee,Tunda ,Baby Madaha na Chid Benz.

Dude alisema makubaliano yakifikiwa watashuti wiki hii huku kambi ikiwa Lamada Hotel.

Baby Madaha ameithibitishia Bongo5 kuhusu kushiriki kwenye mchezo huyo.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents