Burudani

Baby Madaha: Nimewekeza zaidi ya shilingi milioni 500 kwenye kampuni yangu ya filamu (Picha)

Muimbaji na muigizaji wa filamu, Baby Madaha amesema amewekeza zaidi ya shilingi milioni 500 kwenye kampuni yake mpya ya filamu.

2ad00797-5b32-44fb-aa93-e8f5c388619c
Baby Madaha akiwa katika moja ya maduka ya vifaa vya electronics jijini Dubai, UAE

Baby ameiambia Bongo5 leo akiwa Dubai kwaajili ya manunuzi ya vifaa hivyo, kuwa amekuta bei ya vifaa vya uzalishaji wa filamu vimepanda bei maradufu.

“Pesa niliyowekeza mpaka sasa sio chini ya shilingi milioni 500. Vifaa ni ghali sana, especially kamera za kisasa na vitu vingine,” ameongeza.

“Nimejipanga kwa sababu najua nini kinaendelea katika industry. Mimi ninahusika moja kwa moja katika tasnia so nitatumia uzoefu wangu kuyafuta makosa ambayo wengine waliyafanya na wengine wanayaona lakini wanayapuuzia.”

3b0542ee-3c48-4ab1-af07-56a488b4e148

Kwa upande wa muziki, Baby Madaha amewataka mashabiki wake kusubiria ujio wa wimbo wake mpya uitwao Corazon.

“Immediately baada ya uchaguzi kuna bonge la song naliachia linaitwa Corazon maana yake ni moyo. Hiyo ndio funika, na hapo hapo naachia bonge la movie linaitwa Saint & Ghost. Itakuwa two in one, kubwa kuliko kuitambulisha rasmi kampuni yangu mwenyewe ya utayarishaji na usambazaji wa kazi zangu za filamu.”

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents