Baby Powder imekamilika

Baby Powder imekamilika
Watanzania waishiyo Atlanta, USA, wanatarajia kuibuka na movie ijulikanayo kama BABY POWDER ifikapo Novemba 14 ndani ya mwaka huu.

Filamu hii inatarajiwa kuonekana kwa mara ya kwanza kabisa ndani ya jiji la Atlanta lililopo jimboni Georgia nchini Marekani tarehe 14 November,2009.Baada ya hapo itaonyeshwa jijini Houston huko Texas tarehe 26 November,2009 na kisha jijini Washington,DC tarehe 5 December 2009. Baada ya hapo itakuwa zamu ya watu wa Minnesota kuiona tarehe 19 December 2009 kabla ya tour ya Europe na Africa haijaanza tarehe 25 December 2009. Tarehe na miji itakapoonyeshwa filamu hiyo zitatangazwa baadaye.

BABY POWDER ni filamu inayo kugusa maisha ya kweli. PHILIP NKASA (Lambert "LBT" Tibaigana) ni kijana wa kitanzania anakwenda marekani kwa matumaini ya kupata elimu ili kuweza kuboresha maisha yake na ya familia yake nyumbani. Philip ananzaa maisha yake ndani ya marekani katika mji mdogo wa Wichita,KS na baada ya kumaliza shule na kushindwa kupata kazi ,Philip anakata shauri kwenda kujaribu bahati yake katika jiji la Atlanta, GA. Mambo hayawi kama Philip alivyo tegemea upatikanaji wa kazi Atlanta unakua wa shida,ili kuendesha maisha Philip anachukua kazi ya malipo kidogo pamoja na kuaa ana degree…hali ya maisha ya wazee wake inaendela kua mbaya kutokana na mapato yake kidogo anashindwa kuwasaidia,
Baada ya kugundua mfanyakazi mwenzake Mamdo (Albert Levasseur) anafanya biashara haramu, Philip anona nafasi ya kutatua matatizo yake…lakin baada ya kuonja asali anachonga mzinga na kuingia katika biashara  haramu kwa nguvu zote. kutokana na kukua kwa biashara yake Philip anaoneza msaada kutoka kwa vijana wenzake  Tizo ( Carlos Mwaibulla) Chuma (Ulimboka GWAII Mwanjabala) Wesi (Hadji saidia) kwenye wengi hapa haribiki jambo lakini kundi hili linaubadilisha msemo huo….( mengi yana haribika)
Philip anaingia mapenzi na mrembo kuoka Kenya WARIDI (Tuni Ngigi) ambaye anashindwa kumuambia ukweli kuhusu biashara zake,lakini za mwizi arobaini,Waridi anakuja kukundua…

Majina ya waigizaji:

Lambert Tibaigana- PHILIP NKASA
Tuni Ngigi              WARIDI
Carlos Mwaibulla    TIZO
Ulimboka Mwanjabala  CHUMA
Hadji Saidia            WESI
Lydia Mbuah           JOSELYNE
Warda Hassan        JACKEY
Dynamic                DULAH
Albert Levasser       MAMADO
Babu sikare             KAI

na wengine wengi….

BABY POWDER ni filamu inayo elimisha, sikitisha ,furahisha,na kutia moyo…na ni mkasa wa kuburudisha…

Filamu hii haita toka kwenye DVD mpaka mkatikati ya mwaka 2010 nafasi pekee ya kuiona filamu hii ni wakati wa uzinduzi rasimi katika sehemu mbali mbali

kwanza kabisa BABY POWDER itazinduliwa rasimi ATLANTA,GA November 14th 2009, HOUSTON,TX ( November 26th 2009) WASHINGTON DC ( December 5th 2009) MINNESOTA ( December 19th 2009)  tour ya AFRICA/EUROPE kuanzia DECEMBER 25th 2009
tembelea www.jake-productions.com

au angalia

http://www.youtube.com/watch?v=BzeqaExvQZU

Related Articles

Check Also
Close
Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents