Burudani

Bado nakula mashavu na Albam yangu ya Kwanza

MatonyaMsanii wa muziki wa kizazi kipya almaarufu kwa jina la Matonya ambaye anasimama katika nafasi za juu sana kati ya wasanii wanaofanya vizuri nchini, amedai hana pupa na kutoka na albam nyingine kwani shughuli ya albam ya kwanza bado inaendelea kuwapangisha foleni wasanii wengi tu

MatonyaMsanii wa muziki wa kizazi kipya almaarufu kwa jina la Matonya ambaye anasimama katika nafasi za juu sana kati ya wasanii wanaofanya vizuri nchini, amedai hana pupa na kutoka na albam nyingine kwani shughuli ya albam ya kwanza bado inaendelea kuwapangisha foleni wasanii wengi tu wakiwemo wakongwe na hawa wapya wanaoibukia katika gemu.

 

 

 

Bongo5.com iliweza kupiga story na Matonya ambaye aliezea kwa kifupi mafanikio ambayo mpaka sasa ameshayapata kupitia albam yake ya kwanza “naweza kusema albam yangu ya kwanza imeniwezesha kuyanenepesha maisha yangu kwa kiasi flani kama vile nimeweza kujenga kaikulu kangu kule mkoani Tanga (Banga la Hatari), Nina Duka kubwa maeneo ya Ilala linalijishughulisha na uuzaji wa nafaka na vyakula vya aina mbali mbali, Ninamiliki gari mbili zote za ukweli nina Toyota GX 100 pamoja na Starlet nab ado ninaendelea kugonga kopi kwa wadosi kama vile leo nimetoka kuchukua hundi ya shilingi milioni 4.5 pamoja milioni 1.5 alimradi maisha yanaenda Alhamdulillah” alisema Matonya huku sura ikiwa na muonekano wa Ankara.

 

 

 

Msanii huyu ambaye anamilikiwa na kampuni mpya ijulikanayo kwa jina la RESPECT chini ya Big Boss Chief Kiumbe, anaendelea kurekodi albam yake nyingine lakini hana haraka nayo kwani albam yake bado inafanya vizuri sana sokoni,halikadhalika Matonya anafanya vema sana katika upande wa milio ya kwenye simu (Ring Tone), si Tanzania tu bali hata kule nchini Kenya amekuwa wakiwakimbiza ile mbaya.

 

 

 

Mwisho amewataka wasanii wanaochipukia wajaribu kuwa wabunifu zaidi kwani huu utaratibu wa kuga flani kafanya nini unaweza kuwapoteza kabisa, pia amesema mashabiki wakae tayari kumpokea kwani mapema mwakani anatoka rasmi na kazi zake mpya.

Related Articles

Check Also
Close
Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents