Habari

Baharia apotea ajali ya boti Zanzibar, 10 waokolewa

ZAIDI ya watu 10 wameokolewa baada ya Mv Mudathir kuigonga boti ya Uvuvi ya Mv. Ulezi.

ZAIDI ya watu 10 wameokolewa baada ya Mv Mudathir kuigonga boti ya Uvuvi ya Mv. Ulezi.


Katika ajali hiyo baharia mmoja ameripotiwa kupotea baharini karibu na Pwani ya Zanzibar mapema ndani ya wiki hii.


Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mjini Magharibi, Bakari Khatib Shaaban aliyaweka wazi hayo alipokuwa akizungumza na waandishi wa habari jana, alimtaja baharia huyo wa Mv. Ulezi, kuwa ni Khatib Kombo Khatib (25), ambaye hadi sasa hajaonekana tangu akumbwe na mkasa huo na kwamba juhudi za kumtafuta zinaendelea.


Boti hiyo ya uvuvi iligongwa majira ya saa 5 usiku katika eneo la Fungu Karume baada ya meli hiyo ya Mudathir kufungua nanga katika bandari ya Malindi Unguja kwa ajili ya safari ya kwenda jijini Dar es Salaam.


Boti hiyo ilizama ikiwa na vitu mbali mbali na abilia, Faki Maulid (25) mkazi wa Mtoni Kidatu, Ame Salum Khatib (28), mkazi wa Daraja Bovu, Seif Amran Omar (30) wa Kwamtipura, Ramadhan Mkanga Kassim (31) wa Kwamtipura na Hamad Suleiman Omar (25), wa Chumbuni.


Wengine waliokuwamo katika boti hiyo ni Farahani Sulaiman (41), wa Jang’ombe, Omar Mohd Omar (18), Michenzani, Othman Ussi Salum (22), Kwamtipura, Othman Haji Othman (37) na Nahodha wa boti hiyo Mohammed Omar Salum, ambao waliokolewa na mahabaria wa meli ya Mudathir.

Related Articles

Check Also
Close
Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents