Burudani

Bahati asimulia kilichomtokea kwa Lulu

Mapenzi ya Bahati kwa Elizabeth ‘Lulu’ Michael yalimtokea puani.

Muimbaji huyo wa gospel amefunguka kuwa aliwahi kuja Bongo kwa ajili ya kumpata mrembo huyo wa filamu nchini ili amweke kwenye video ya wimbo wake ‘Maria’ lakini ilishindikana ndipo alipoamua kumtumia Jokate kama model kwenye video hiyo.

“Hii ni siri ambayo nadhani hata Wakenya hawakujua, AY peke yake ndiye alijua. Nilitoka Nairobi kuja hapa [Dar es Salaam] natafuta connection na Lulu kwasababu nataka awe kwenye ile video [Maria] ambayo nimemweka Jokate. Nimekaa kwa hotel Lulu amekataa kushika simu mpaka ikafika mahali nikamwambia ukija kuniona Mungu atakubariki, siku ya pili akakataa kabisa nikamwambia mshikaji AY acha tu nirudi nyumbani. Nikarudi hivyo,” Bahati amesema hayo kupitia Magic FM.

Bahati ameongeza kuwa sababu ya kufanya kazi na Ray Vanny katika wimbo wao mpya ‘Nikumbushe’ ilikuwa ni mipango yake ya muda mrefu ili muziki wake uweze kupata tobo hapa nchini.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents