Habari

Bajeti ya milioni 80 ya mazishi ya Akwilina yawa gumzo mtandaoni

Bejeti ya milioni 80 ya mazishi ya mwanafunzi wa Chuo cha Taifa cha Usafirishaji (NIT), anayedaiwa kuuawa na polisi wiki iliyopita, Akwilina Akwiline, imekuwa gumzo katika mitandao ya kijamii.

Familia hiyo imeikabidhi serikali bajeti ya maziko ya zaidi ya Sh milioni 80 baada ya serikali kusema itagharamia mazisho hayo.

Msemaji wa Familia, Festo Kavishe amekabidhi bajeti hiyo leo Jumanne Februari 20, kwa Katibu Mkuu wa Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia, Dk. Leonard Akwipalo na Mkuu wa Wilaya ya Ubungo, Kisali Makori.

“Hayo ndiyo makubaliano ya familia, tumewakabidhi wataenda na kujadiliana kisha tutakutana nao saa 10 jioni leo, kisha watatueleza ya kwao pia, tunachohitaji ndugu yetu apumzike kwa amani,” amesema Kavishe.

Baada ya kukabidhi bajeti hiyo kwa serikali, wadau mbalimbali wa mambo katika mitandao ya kijamii wamekuwa wakiijadili bajeti hiyo. Haya ni baadhi ya maoni ya wadau hao katika mitandao ya kijamii.

G de Don
Mbn pesa kidogo ivo!
Naiomba familia iwe serious bas msifanye bajeti kwa woga tulizeni akili hiyo ni kwa ajili ya mazishi bado mambo kadha wa kadha ya msiba na familia

Maimuna Mohamed
Kabsa mana wakat unatoa gharama zako kumsomesha mtoto wako ina mana kwmba ni kwa faida yake na ya mzazi pia hta kma roho ya mlengwa haitorud kma wao wamewakomoa familia ya marehemu bac na familia ina haki ya kuamua chchte tna hyo ndgo wangesema hta million 150 angalau hv wanajua mpka hpo marehemu alipofikia ameshatumia gharama shs ngpi?Kwanza wazaz wake wameshakuw wazee ni bora wapewe hzo fedha ziwafae uzeeni..nyie mnaosapot serikali halijawah kuwakuta ndo mana.

OG Dogo Maginga Tz
Mmmmmh mil80 yote duh 😊😊R. I. P Mdogo wangu huku umeacha watu kupiga dili wachaga hawapendi ujinga hii inaitwa kufa kufaana.

Kelvin Korosso
Watu wa hajabu kweliii hii familia yaanii mnafurahi mwanenu kufa ilmradi mpate mihelaa iyo mmegeuza kifo cha mwanenu mtajiiiii?? hama kweliii umaskini kitu kibaya saana nimeamini!!

John Hizza
Hiyo ni bajeti yao musiwaingilie kama mumeshindwa kugaramia kama ahadi yenu mulioitoa basi changieni na ijulikane kuwa niwachangiaji tuh hamkugaramia garama yote kama ahadi yenu mulioitoa kimhemko

Vivquetyviv Viv
Serikal iwe makini ..kwa bajeti hii mnakula chakula gan njiani cha mill 3 ..uko rombo mnakula nn mill 30 mwisho wa siku msiba ukiisha mnaaza kugombana mwenyewe

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents