Burudani ya Michezo Live

Bajeti ya usajili Man United msimu huu ni pasua kichwa, sawa na dau la Ronaldo kwenda Juventus

Meneja wa Manchester United, Ole Gunnar Solskjaer amekabidhiwa pauni milioni 100 pekee kwaajili ya kufanya usajili kwenye dirisha hili kiasi ambacho ni kidogo mno na si kawaida.

Image result for ole gunnar solskjaer in bad feeling

Kwa mujibu wa chanzo cha ndani ya United, kimeuwambia mtandao wa michezo wa ESPN FC kuwa United imetoa kiasi hicho kwaajili ya usajili kwenye kipindi hiki huku ikitegemea kuuza baadhi ya nyota wake ili kuongeza pato hilo.

Bajeti hiyo ni sawa na usajili wa mchezaji mmoja wa Juventus, Cristiano Ronaldo aliyetoka Real Madrid kwa dau la pauni milioni 105.  Nyota hao wanaotegemewa kuondoka na huwenda kusaidia usajili huo ni pamoja na Paul Pogba, Romelu Lukaku na David De Gea ambao wamehusishwa kutimka.

Hata hivyo imeshuhudiwa Ander Herrera na Antonio Valencia wakiondoka kama wachezaji huru mwishoni mwa msimu, miezi mitano baadae kuuzwa kwa Marouane Fellaini kwa dau la pauni milioni 10.5 kwenda Shandong Luneng, Solskjaer amesikika akisema kuwa anahitaji kukitengeneza kikosi hicho.

Solskjaer ambaye amekabiziwa rasmi timu hiyo mwezi Machi akichukua mikoba ya Jose Mourinho baada ya kutimuliwa Disemba mpaka sasa amemsaini aliyekuwa winga wa Swansea City, Daniel James.

United mpaka sasa imemuongezea mkataba, Ashley Young, Phil Jones, Chris Smalling na Juan Mata pia kumuongeza beki wa kati wa Leicester na timu ya taifa ya Uingereza, Harry Maguire, kiungo wa Newcastle United, Sean Longstaff na beki wa Crystal Palace, Aaron Wan-Bissaka. Hata hivyo vijana hao wa United wanatarajiwa kurejea kwaajili ya msimu mpya wa ligi Julai 1 huku wakiwa imetumika pauni milioni 15 mpaka sasa.

Related Articles

Back to top button
Close
Bongo5

FREE
VIEW