Habari

Balozi Slaa, Mboweto wamuaga Makamu wa Rais (+Picha & video)

Balozi wa Tanzania nchini Nigeria, Mhe. Muhidin Ally Mboweto pamoja na Balozi wa Tanzania nchini Sweden Mhe. Wilbrod Peter Slaa leo wakutana na Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan kwenye makazi yake Oysterbay, jijini Dar es Salaam kwa lengo la kumuaga tayari kwenda kwenye vituo vyao vipya vya kazi.

Mabalozi hao ambao waliapishwa jana na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli Ikulu jijini Dar Es Salaam.

Makamu wa Rais aliwatakia safari njema huko waendapo kwenye vituo vipya vya kazi ambapo aliwasihi kwenda kufanya kazi kwa moyo mmoja na kuzingatia maelekezo ya Mhe. Rais

“Hakikisheni mnaitangaza nchi yetu vizuri na kuwashawishi wawekezaji ili waweze kuja kwa wingi, nchi yetu ina fursa za kutosha” alisema Makamu wa Rais.

Kwa upande wao Mabalozi hao walimuahidi Makamu wa Rais kuiwakilisha nchi vizuri na kufanya kazi kizalendo.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents