Habari

Balozi wa Hennessy atua nchini kuelimisha matumizi ya kinywaji hicho

Balozi wa Hennessy Cyrile Gautier Auriol

Balozi wa kinywaji cha Hennessy, Cyrile Gautier Auriol, jana alizungumza na waandishi wa habari na kuwafahamisha namna kinywaji hicho cha Hennessy kinavyotumika. Balozi huyo aliwasili juzi usiku kwa ziara ya siku mbili jijini Dar es Salaam ikiwa ni katika ziara yake ya siku tano katika ukanda wa Afrika Mashariki.

Dhumuni ya ziara yake ni kuwazawadia wanywaji wa Hennessy pamoja na kuwaelimisha na kujenga uelewa kuhusu utumiaji wa vinywaji vya kampuni hiyo katika ukanda huu wa Afrika Mashariki.

Ziara hii ya balozi Auriol ni ya pili hapa nchini ndani ya miezi 12, hali inayoonyesha ukuaji wa matumizi ya kinywaji hicho hapa nchini na katika nchi za Afrika Mashariki kwa ujumla.

Akiongea na waandishi wa habari Bwana Auriol alisema Hennessy ni kinywaji kinachopendwa zaidi duniani, kikiwa naa historia ya miaka 250, zaidi ya hapo kinatengenezwa katika eneo la Cognac kaskazini mwa nchi ya Ufaransa, na hapa nchini kinywaji hiki kimekuwa kwenye soko kwa muda mrefu na huku watumiaji wake wakiongezeka siku hadi siku

Balozi huyo alisema katika ziara yake hiyo ya siku mbili nchini, Auriol atakutana na wapenzi wa Hennessy katika matukio mbalimbali maalumu ikiwemo chakula cha mchana katika hoteli ya Hyatt Regency ambapo baadhi ya wageni maalum ikiwemo wanawake watapata fursa ya kujifunza historia ya kinywaji cha Hennessy lakini pia kuonja aina mbalimbali za kinywaji hicho lengo likiwa kuwafundisha wanawake namna ya kufurahia kinywaji hicho wakiwa majumbani mwao.

Balozi Auriol pia atahudhuria chakula cha jioni na wafanyabiashara wa hapa nchini katika mgahawa wa Akemi uliopo katika ghorofa la Diamond Jubilee. Balozi Auriol atatoa elimu kuhusu Hennessy ikifuatiwa na uonjaji wa kinywaji hicho pamoja na chakula kitakachoandaliwa na mpishi mkuu wa hotel hiyo.

Ziara ya balozi Auriol inaenda sambamba na juhudi nyingine za kutangaza kinywaji hicho hapa nchini, mojawapo ikiwa ni kampeni ya mabango ya ‘Flaunt Your Taste’ yaliyosambaa jiji zima pamoja na ukamilishaji wa chumba cha Hennessy kilicho katika Club 327, ambacho balozi Auriol atakizindua.

Balozi Auriol atakuwa na kikao maalumu pia na wapenzi wakubwa wa kinywaji hicho, na pia atawazawadia mialiko maalumu ya kuingia kwenye klabu ya wapenzi wa kinywaji hicho ya Afrika mashariki.

Lakini jambo kubwa zaidi ambalo Auriol atalifanya ni kutoa mafunzo maalumu kwa baadhi ya wahudumu kutoka katika bar kubwa ambayo yatagusa sio tu katika uchanganyaji sahihi wa kinywaji cha Hennessy bali pia historia fupi na aina tofauti za kinywaji hicho.

Lengo kuu la mafunzo hayo yatakayofanyika katika hoteli ya Southern Sun na George & Dragon ni kuwapa wahudumu ujuzi utakaowawezesha kutoa huduma bora na ya kipekee kwa wateja wao wakati wakiburudika na kinywaji cha Hennessy kwenye bar au hotel wanazozipendelea.

Ziara ya balozi Auriol itahitimishwa na uonjaji na ulinganishaji wa kinywaji cha Hennessy katika ukumbi wa nje wa hoteli ya Serena. Katika sherehe hiyo Auriol atawaelimisha na kuwaburudisha wageni maalumu wakiwamo wanamitindo maarufu, waandishi na wafanyabiashara katika usiku wa vinywaji, chakula na burudani.

Kuhusu Hennessy

Hennessy ni kinywaji chenye historia ndefu na ya kipekee. Kwa miaka mingi Hennessy imejikita kwenye asili yake, huku ikijivunia historia ya mwanzilishi wake, Richard Hennessy, ambaye mwaka 1765 alianzisha kampuni hii kwenye fukwe za Charente.

Kwa zaidi ya miongo minane, familia ya Hennessy imezunguka dunia nzima kuitambulisha Hennessy kwa wanywaji ambao sasa wamekuwa wapenzi wakubwa wa kinywaji hicho.

Hadi leo, Hennessy inatengenezwa kwa umakini ule ule, na familia ile ile tokea karne ya 19, huku ikifurahiwa na wanywaji duniani kote.
Unywaji wa Kiistarabu

Kampuni ya Hennessy inazingatia unywaji wa pombe wa kistaarabu na inashauri wanywaji wa Hennessy kunywa kwa kiasi na kwa kuzingatia miongozo iliyopendekezwa ya kiasi cha pombe kwa siku.

Related Articles

Check Also
Close
Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents