BurudaniMitindo

Balozi wa Redds kusakwa jana

Kinyanyanyiro  cha kumsaka Balozi wa Redds kilifanyika jana katika fukwe ya mbalamwezi  Mikocheni jijini Dar es Salaam ikiwiwahusisha walimbende 30 kutoka kambi ya Miss Tanzania 2010.

 

Meneja chapa wa kinywaji cha Redds Kabula Nshimo alisema kigezo kikubwa  kubwa  cha kumpata wa Balozi wa Redds  ni mrembo mwenye, tabasamu nzuri, uelewa wa hali ya juu na  kuwa mbunifu katika fani ya ulimbwende.

Walibwende hao walipita jukwaaani wakiwa wamevalia mavazi ya wabunifu tofautii wa hapa nchini, ikiwa ni moja ya mashindano.

Kabula alisema mshindi wa Balozi wa Redds atatangwazwa siku ya sherehe ya kumtafuta mlimbwende wa Miss Tanzania 2010 itakayofanyika Septemba 11 katika ukumbi wa Mlimani City.

Sherehe hiyo iliambatana na burudani kabambe kutoka kwa bendi ya Tanzanite, sambamba kabisa na mshereheshaji mahiri Jokate Mwengelo.

Pia ilihudhuriwa na Balozi wa Redds 2009 Victoria Martin, Nancy Sumari na Irene Kiwia kutoka kampuni ya Frontline Managment ambao ndio walikuwa waratibu shughuli hiyo.

Related Articles

Check Also
Close
Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents