Tupo Nawe

Banana Zoro: Kuoa kunasaidia msanii kutoyumba kimaisha

Muimbaji wa muziki, Banana Zoro amesema maisha ya kisanii yamejaa vishawishi na anasa kibao kiasi kwamba inawawia vigumu wasanii mabachela (ambao hawajaoa) kufanya mambo ya msingi katika maisha.

banana Zoro

Banana ameiambia Planet Bongo ya East Afrika Radio kuwa yeye mwenyewe ni mfano wa hilo, kabla ya kuoa maisha yalikuwa tofauti sana na sasa.

Amesema maisha ya msanii yamejaa vishawishi kibao ambavyo unahitaji mke wa kuhakikisha havikuyumbishi kimaisha.

kuhusu video ya ngoma yake mpya ‘kaseme Tena’, Banana amesema anatarajia itatoka mwishoni mwa mwez huu au mwanzoni mwa mwezi wa Pili. Anatarajia itakua video ya #kitanzania zaidi na mpango uliopo ni kushoot mkoani Dodoma.

Credit: @dullahplanet (Instagram)

Related Articles

Back to top button
Close
Bongo5

FREE
VIEW