Promotion

BancABC Yazindua Akaunti Maalum Na Ya Kipekee!

JIONGEZE MARADUFU. Pata riba hadi asilimia kumi na sita (16%)kwa mwaka katika amana hii na kujipatia fursa ya kukopa dhidi ya amana yako.

Dar Es Salaam, Machi 14 2017: BancABC, ambayo ni sehemu ya Atlas Mara, leo imezindua bidhaa adimu itakayokuwezesha kuvuna riba hadi asilimia 16% kutokana na akiba maalum utakayojiwekea.

Katika hali ya kawaida kama tulivyozoea, amana za muda maalum zimekuwa kivutio kwa wateja wengi wa mabenki. Kwa kuanzia amana hii yenye riba kubwa ni nzuri kuliko kufungua akaunti ya akiba ya kawaida kwani unapata riba nzuri zaidi.

Faida nyingine ni uhakika wa mapato ya riba na uwezo wa kuamua namna gani ya kuitumia, kukopa au kuweka akiba zaidi, utakavyopenda mwenyewe.

BancABC imechukuwa hatua kubwa zaidi kwa kutoa riba ya asilimia 16%, vilevile utapata riba hii bila ubabaishaji.

Akiongea jijini Dar es Salaam katika mkutano na waandishi wa habari kwenye makao makuu ya benki hiyo, Mkuu wa kitengo cha wateja wadogo wadogo na wale wafanyabiashara wa kati. Mama Joyce Malai alisema hakuna tena nafasi nzuri ya kunufaika na huduma za benki kama hii iliyopo sasa.
“Tunathamini mchango mzuri wa wateja wetu, kwa hiyo kama benki makini kupata ruzuku tunatoa huduma hii ya kipekee kama zawadi maalum”.

Hii haina tofauti ya kupata faida ya biashara hata kabla hujaianza! Tunaamini tumeileta huduma hii kwa wakati muafaka, katika muda inayohitajika haswa. Tuna hakika bidhaa hii mpya ya kibenki itawavutia wateja wengi hasa wale walio makini”, alisema Joyce.
“Riba ya asilimia16% inayolipwa kabla hujamaliza muda wa kuweka akiba, ni kivutio kikubwa, ambacho kitamfanya mteja ajivue majukumu makubwa ikiwa pamoja na kulipa ada za shule, kodi ya nyumba, usafiri au kuitumia kama mtaji kwenye biashara zingine azipendazo kwa kuchukua mkopo ambao dhamana ni amana yako kaika benki hapo kwa hapo.

“Vile vile nawasihi wale wote ambao hawana akiba na BancABC kutumia nafasi hii na kufaidika kwa kufungua akaunti na kupata maelezo zaidi juu ya faida ya huduma hii ya kipekee. BancABC iko makini kukutana na wateja wake ili kujenga misingi ya mafanikio ya pamoja“, alimalizia.
BancABC ipo tayari kutoa huduma hii kwa wateja wake na wasio wateja kuanzia leo kwa miezi miwili.

Kwa maelezo zaidi Piga 0779111000 au Email: [email protected]
……
KUHUSU KAMPUNI YA ABC
Kampuni tanzu ya ABC Holdings Limited ni shirika mama la mabenki mbalimbali chini ya nchi zilizopo kusini mwa jangwa la Sahara zinazotoa huduma kwa kupitia bidhaa ya BancABC ambayo hutoa huduma mbalimbali za kifedha zikiwemo za kibinafsi, biashara na makampuni ya kibenki, pamoja na umilikaji bora wa mali, udalali wa hisa, na uwekaji hazina ya pesa.
Katika mwaka 2014, Atlas Mara ilichukua hisa kubwa ndani ya ABC Holdings. Ikijivunia ufanisi bora wa kitaaluma, rasilimali watu, itikadi, ubunifu, mahaba ya uadilifu, , BancABC inaendelea kujiweka mahali bora ili kupata muonekano wa kuwa benki ya kuvutia wateja wengi barani Afrika kwa kutoa huduma zenye kiwango cha kimataifa duniani kote na kuwa mfumbuzi wa matatizo yote ya kifedha kukidhi matakwa ya wadau wake.

www.bancabc.com

KUHUSU ATLAS MARA
Atlas Mara imeorodheshwa katika soko la hisa la London mwezi Desemba 2013. Atlas Mara ina mtazamo wa kuwa taasisi itakayokuwa bora kusini mwa jangwa la Sahara kwa kutoa huduma bora za kifedha kupitia uzoefu mkubwa kitaaluma, uzoefu wa kupata mitaji, uwezo wa kifedha na kutoa huduma za kifedha vile vile. Malengo yake ni kutumia uzoefu na ujuzi wa kimataifa kwa ushirikiano na maono ya wenyeji kwa kuunga mkono maendeleo ya kiuchumi katika nchi ambazo kampuni inatoa huduma zake.
www.atlasmara.com

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents