Tupo Nawe

Bangi inayopatikana mtaani nchini Uhispania yatajwa ‘kuwa na kiwango kikubwa cha chembe chembe za kinyesi’

Bangi inayouzwa katika mitaa ya Madrid ina viwango vya hatari vya kinyesi utafiti umeonyesha. Chembe chembe za bakteria ya E.coli na kuvu ya Aspergillus zimegunduliwa na wakaguzi waliofanyia uchunguzi sampuli 90 zilizonunulia ndani na katika maeneo yanayopakana na mji mkuu huo wa Uhipsania.

Sampuli za Hashish zilizofungwa kwenye mifuko ya plastiki ndio zilizogunduliwa kuwana viwango vikubwa zaidi, inaarifiwa ni kutokana na namna zilivyoingizwa nchini.

Kwa mujibu wa BBC. 40% ya hizi zina harufu za kinyesi, mhariri mkuu wa utafiti huo ameeleza.

Kununua, kuuza, na kuingiza bangi ni marufuku nchini Uhispania kama vile ilivyo kinyume cha sheria kuivuta hadharani – licha ya kwamba ni halili kuikuza kwa mataumizi binfasi , ili mradi haionekanai wazi, na inatumika kwa faragha.

Utafiti ulifanywa vipi?

José Manuel Moreno Pérez, mtafiti kutoka chuo kikuu cha Universidad Complutense mjini Madrid, alikusanya hashish inayofahamika kwa jina maarufu mitaani kama hash au resin kutoka kwa wauzaji maarufu mitaani mjini na katika viunga vyake.

Lengo ilikuwa ni kubaini iwapo mihadarati hiyo infaa kutumika na binaadamu.

Kundi lake la watafiti baadaye wakazigawanya sampuli kwa umbo, la namna zilivyoundwa kuona iwapo umbo moja lina uchafu huo ikilinganihswa na jingine.

Utafiti huo umechapishwa katika jarida la Forensic Science International.

Tahadhari yatolewa uhispania kuhusu bangi iliyopakwa kinyesi kwa maksudi

Utafiti unasema nini?

Wamegundua kwamba baadhi zina 93% ya viwango vya hatari vya bakteria ya E.coli na nyingine zikiwana kiwango cha 29.4% cha bakteria hiyo.

10% ya sampuli hiyo ya bangi pia ziligunduliwa kuwana kuvu hatari ya Aspergillus, inayoweza kusababisha matatizo makubwa kiafya.

Kati ya 88% ya sampuli zilizofanyiwa ukaguzi zimegunduliwa kuwa hazifai kutumiwa na binaadamu.

Coloured scanning electron micrograph (SEM) of Escherichia coli 0157:H7

Hatari yake ni ipi kando na kuwa na uchafu?

Kwa mujibu wa utafiti, hatari inayotokana na bakteria ya E.coli na kuvu ya Aspergillus ni kubwa mno kiasi cha kufanya uuzaji bangi mitaani kuwa ni suala linalohusu afya ya umma.

Maambukizi ya E.coli kwa mfano yanaweza kusababisha kuharisha, kutapika maumivu ya tumbo homa na kuvuja damu katika kinyesi – na kwa baadhi ya watu hili linaweza kusababihsa matatizo mengine makubwa zaidi ya afya.

Vilevile, mtu anapoinusa kuvu ya Aspergillus inawezakusababisha matatizo makubwa kwa watu ambao ayari mfano wana matataizo ya mapafu, kama pumu au katika watu walio na kinga ndogo mwilini. Utafiti unaeleza kwamba hii ni hatari kubwa zaidi kwa wagonjwa wa saratani ambao kwa mara nyingine huhitajika kuvuta bangi kusaidia katika matibabu ya chemotherapy.

By Ally Juma.

Related Articles

Back to top button
Close
Bongo5

FREE
VIEW