Burudani

Bantu Music waja na mradi wa ‘16 Bars Mixtape’

Studio ya muziki ya Bantu Music ya Dar es Salaam inatarajia kuja na mradi wa ‘16 Bars Mixtape.’

20151207015610

Taarifa ya producer wa studio hiyo, No Future imesema:

Ni mradi mpya kutoka studio kubwa za Bantu Music. Mradi ambao umehusisha wasanii tofauti Wa miondoko ya Hiphop pamoja na RNB.

Mradi huu umehusisha mfumo tofauti wa ufanyaji kazi kwa kutengeneza wimbo wenye mistari 16 (kumi na sita) kwa kila msanii aliyehusika.

Ni mradi endelevu utakaokuwa ukitoka kwa awamu tofauti. Kwa kila wimbo uliofanyika una video yake na video hizo zitakua zikitoka kwa muda tofauti.

Mradi huu umeandaliwa na studio za Bantu music. Watayarishaji mbalimbali wamehusika kuandaa kanda mseto hii.

Utayarishaji Wa mradi huu kwa awamu ya kwanza umekamilika nyimbo zitaanza kutolewa hivi karibuni.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents