Banzastone taabani

Banzastone taabani
Mtunzi na muimbaji mahiri wa nyimbo za muziki wa dansi nchini, Ramadhani Masanja ‘Le General Banzastone’, au ukiweza mwite ‘Mwalimu wa Walimu’ amelazwa katika Hospitali ya Wilaya ya Mwananyamala iliyopo Kinondoni, jijini Dar es Salaam

Habari
kutoka chanzo cha kuaminika zimesema msanii huyo yuko hoi na amelazwa
katika hospitali hiyo mwanzoni mwa wiki hii kwa matibabu.

“Hali ya Banzastone ni mbaya, amedhoofu mno hali inayopelekea kuonekana
kana kwamba amechanganyikiwa hivyo mipango inafanywa apelekwe katika
hospitali ya wagonjwa wa akili ya Mirembo iliyoko mkoani Dododma,”
kilisema chanzo hicho.

Hii itakuwa ni mara ya pili kwa msanii huyo kuumwa na kuwa taabani,
mara ya kwanza aliugua hadi akasingiziwa kuwa kafa mwaka 2006 ambapo
aliibuka na albamu ya ‘Hujafa Hujasifiwa’ wakati huo akiwa ni
mwanamuziki wa Bendi ya Twanga Chipopolo.

Related Articles

Check Also
Close
Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents