Moto Hauzimwi
Shinda na SIM Account

Bao la ushindi la mgharimu beki wa Chelsea

Mchezaji wa klabu ya Chelsea, Antonio Rudiger ameonyesha kuumia mguuni baada ya kuipatia bao pekee na laushindi timu yake katika mchezo wa Ligi Kuu nchini Uingereza hapo jana dhidi ya Swansea.

Katika mchezo huo uliyomalizika kwa Chelsea kuibuka na ushindi wa bao 1-0 lililofungwa na difenda wake, Rudiger katika dimba la Stamford Bridge umemalizika huku mchezaji huyo akionyesha kuvuja damu baada ya kuvua kiatu chake.

Kupitia mtandao wake wa kijamii wa Instagram, Antonio Rudiger amepiga picha na kuonyesha namna alivyo umia huku akitupia lawama kampuni ya Nike kwa viatu walivyompatia.

“Nike, nikitu gani hiki?.” Ameandika Rudiger

Licha ya kuonekana kuvuja damu katika mguu, Rudiger haikumuathiri kushindwa kucheza dakika zote 90 za mchezo.

Meneja wa kikosi hicho, Conte amesema kuwa walihitajika kupata goli la mapema na kwakushindwa kufanya hivyo kumawalazimu kutumua jitihada nyingi ili kupata bao.

Leave a comment

Related Articles

Bongo5

FREE
VIEW