Michezo

Bara la Afrika linaweza kutoa idadi kubwa ya waamuzi kombe la dunia 2018 – Wambura

Makamu Rais wa Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF), Michael Wambura amesema, kuna uwezekano mkubwa Bara la Afrika, likatoa idadi kubwa ya waamuzi katika fainali za michuano mikubwa hususani Kombe la Dunia.

Makamu Rais wa Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF), Michael Wambura

“Kuna uwezekano mkubwa Bara la Afrika, likatoa idadi kubwa ya waamuzi katika fainali za michuano mikubwa hususani Kombe la Dunia.” Amesema Makamu Rais wa TFF, Michael Wambura.

Wambura ameongeza “Waamuzi wa Afrika wana uwezo. Ninyi wakufunzi ni wa kufanya waamuzi wetu kuwa na uwezo zaidi. Ni aibu kwa Bara kubwa kama Afrika lenye nchi wanachama 54 wa FIFA kuwa na waamuzi wachache katika fainali za Kombe la Dunia.

Wambura amesema hayo hapo jana siku ya Jumanne wakati akifungua kozi ya Wakufunzi wa Waamuzi kutoka sehemu mbalimbali barani Afrika kat Ukumbi wa ILO, Dar es Salaam.

Kozi hii ya wiki moja ya waamuzi hatua ya tatu ‘Futuro III’ inayofanyika hapa nchini inajumuisha nchi 26 ambapo inajumla ya washiriki 58 kutoka mataifa  mbalimbali ikiwemo mwenyeji Tanzania huku jumla ya wakufunzi sita wakitokea Shirikisho la soka duniani FIFA akiwemo Carlos Henriques na Dominic Chiellens.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents