Habari

Barabara iliopo chini ya bahari visiwani Zanzibar kuboreshwa zaidi

Barabara ambayo iko chini ya bahari na ni kiungo muhimu kwa wakazi wa kisiwa kidogo cha uzi kilioko mkoa wa kusini Unguja na mji wa Zanzibar inatarajiwa kuimarika baada ya serikali kutoa fedha na vifaa vya ujenzi.

Hali hiyo inatokana na ziara ya Katibu Mkuu Wizara ya Usafirishaji, Mawasiliano na ujenzi Mustafa Aboud Jumbe ambaye ndiye aliyefanikisha kutoa msaada huo utakaowezesha barabara hiyo ambayo iko baharini na inatumiwa na wakazi kwa miguu na usafiri wa barabara wakati maji ya bahari yanapotoka baharini yanapokuwa ambapo akiongea katika eneo la tukio akiwa amefuatana na viongozi wa serikali katibu huyo amesema hilo ni jukumu la serikali inapoona msaada unahitajike hatua kama hizo ziungwe mkono.

Nae mkandarasi wa kijijini hapo ambaye amewaunganisha wakazi wa kijiji hicho kuitengeneza barabara hiyo yenye urefu wa kilomita mbili kwa kuweka mawe na kutandika zege Shaya Mohamed Haji ambapo amesema kazi hiyo itamalizika katika kipindi cha mwezi mmoja na kuishukuru serikali kupitia kwa katibu mkuu huyo kuona umuhimu na kujali kilio cha wakazi wa Uzi, huku mmoja ya wazee wa kisiwa hicho mzee Haji amesema wataendelea kutoa ushirikiano ili wafanikishe lengo hilo.

Barabara hiyo ya Uzi ambayo iko baharini ndio njia pekee ambayo wakazi wa kisiwa hicho hutumia kuja mjini Zanzibar ambapo wanalazimika kuondoka kisiwani saa nne asubui na kama kurudi iwe kabla ya saa kumi ili kuwahi maji ya baharini kabla hayajarudi na kuifunika barabara hiyo.

Source: ITV

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents