Siasa

Barabara kuu zote kuwekewa lami

Rais Jakaya Kikwete amesema serikali imedhamiria kuzijenga kwa kiwango cha lami barabara zote kuu, za mikoa na zile za vijijini ili kurahisha usafiri na usafishaji wa bidha na kuharakisha maendeleo ya wananchi na taifa

Rais wa Jamuhuri ya muungano wa Tanzania Mheshimiwa Jakaya Kikwete amesema serikali imedhamiria kuzijenga kwa kiwango cha lami barabara zote kuu, za mikoa na zile za vijijini ili kurahisha usafiri na usafishaji wa bidha na kuharakisha maendeleo ya wananchi na taifa kwa ujumla.


 


Hayo aliyasema alipokuwa mkoani Mwanza kwenye uzinduzi wa barabara ya Geita Buzilrayombo Kyamyorwa iliyojengwa kwa kiwango cha lami, na wakati wa uzinduzi wa ujenzi wa barabara ya Usagara- Geita inayoanza kujengwa kwa kiwango cha lami inayotarajiwa kukamilika mwaka 2010.


 


Amesema katika kipindi cha miaka michache ijayo serikali inatarajiwa kukamilisha mpango wa kuiungaisha Tanzania na nchi jirani za Kenya, Uganda, Rwanda Burundi na Jamhuri ya Kidemokrasi ya Kondo kwa mtandao wa barabara za lami mpango ambao unaojumuisha mtandao wa barabara za ukanda wa ziwa Victoria na mtandao barabara za ukanda wa kati na kusini.


 


Mapema Waziri wa Miundombinu Dakta Shukuru Kawambwa alisema azma ya serikali ya kujenga kwa kiwango cha lami barabara ya kutoka Mtwara hadu Mtukula mkoani Kagera iko mbioni kufikiwa, kwani hadi sasa ni kilomita 290 tu zilizosalia katika kilomita 2130, na kwamba hatua hiyo itafikiwa mwaka 2010.


 

Related Articles

Check Also
Close
Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents