Habari

Barabara ya Kivule yaanza kujengwa mara baada ya RC Makonda kuwasweka ndani makandarasi – Picha

Barabara ya Kivule yaanza kujengwa mara baada ya RC Makonda kuwasweka ndani makandarasi - Picha

Baada ya makandarasi wanaojenga barabara ya Kivule kuswekwa ndani na mkuu wa mkoa wa Dar Es Salaam hatimaye Kampuni ya Ujenzi ya Nyanza imeanza ujenzi wa Barabara ya Kitunda-Kivule, Ukonga Dar es Salaam.

Makonda alitoa amri hiyo ya Wakandarasi wa kampuni hiyo kukamatwa mara moja Dar es Salaam Alhamisi ya tarehe 24 mwezi octoba mwaka 2019, baada ya kampuni hiyo iliyopewa zabuni ya kuchelewa kuanza ujenzi licha ya kulipwa malipo ya awali ya sh. bil. 4.8. Mkataba wa ujenzi umeanza Oktoba Mosi.

Akizungumza na vyombo vya habari, RC Makonda alisema kuwa wakandarasi hao, watakuwa akienda kujenga barabara hiyo wakitokea mahabusu.

Pilikapilika za ujenzi zimeanza ijumaa katika eneo la Kitunda, ambapo yalionekana makatapila yakikwangua sehemu ya barabara hiyo, huku mengine yakisawazisha vifusi vilivyokuwa vinamwagwa na malori.

Kampuni hiyo itajenga kwa kiwango cha lami kipande cha barabara chenye urefu wa km 3.2 kuanzia Kituo cha Polisi Kitunda hadi Mwembeni.

Ubovu wa barabara hiyo ya kutoka Banana, Kitunda hadi Kivule Fremu Kumi, imekuwa ni kero na kilio cha muda mrefu kwa wakazi wa eneo hilo. Ujenzi wa kipande hicho cha barabara unatarajiwa kukamilika Oktoba mwakani.

Kila msimu wa mvua kama huu barabara hiyo uharibika na kuwa na mshimo yanayosababisha daladala nyingi kusita kwenda huko, hali ambayo inawafanya abiria kulipa kiasi kikubwa cha nauli hadi sh.3000 kutoka Banana hadi Flemu Kumi kwa kutumia usafiri wa Bajaji na Bodaboda.


Wakazi wa eneo hilo wameiomba serikali kuwaonea huruma kwa kuhakikisha ujenzi wa kipande hicho kukamilika haraka kabla ya mvua za masika, lakini pia kumalizia kipande kingine cha barabara kutoka Mwmbeni hadi Flemu kumi.
Chanzo Michuzi
By Ally Juma.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents