Habari

Barack Obama aja kimya kimya Tanzania na kuacha ujumbe mzito serikalini (+video)

Barack Obama aja kimya kimya Tanzania na kuacha ujumbe mzito serikalini (+video)

Rais wa zamani wa Marekani, Barack Obama leo Julai 5, 2018 ameondoka nchini Tanzania baada ya kutimiza ziara yake ya kimya kimya ya mapumziko katika Hifadhi za Taifa za Serengeti zilizopo mkoani Mara.

Barack Obama na Waziri wa Mambo ya Nje, Ushirikiano wa Kimataifa, Mhe. Augustine Mahiga

Waziri wa Mambo ya Nje, Ushirikiano wa Kimataifa, Mhe. Augustine Mahiga akimlaki Obama katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Kilimanjaro (KIA) amesema kuwa Obama alikuja nchini siku 8 zilizopita na yeye ndiye aliyempokea lakini Rais huyo mstaafu hakutaka taarifa zisambae kwani alihitaji awe faragha zaidi.

Kwa upande mwingine, Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro, Mhe. Anna Mghwira amesema kuwa kwa dakika moja aliyoongea naye, Obama amesema Serikali lazima ijitahidi kuvitangaza vivutio vyake kimataifa kwani, inavivutio vingi sana lakini watu hawavijui. Tazama video hapa chini akilakiwa

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents