Habari

Barack Obama ‘arusha vijembe’ kwa Rais Donald Trump

Rais wa zamani wa Marekani, Barack Obama ameukosoa uongozi wa sasa wa Marekani kwa kusema kuwa siasa za sasa nchini humo ni za kibaguzi na za hofu huku akishindwa kumtaja moja kwa moja Rais Donald Trump.

Rais wa zamani wa Marekani, Barack Obama na Jim Murphy mgombea Ugavana jimbo la New Jersey.

Akiwa kwenye kampeni za kuwapigia debe Wagombea wa ugavana kwa tiketi ya chama cha Democratic wa jimbo la New Jersey na Virginia, Barack Obama amesema kwa sasa Wamarekani wana kila wajibu wa kumpigia kura kiongozi ambaye hatakuwa na siasa za kuwagawa  kwa namna yoyote ile.

Kitu ambacho hatuwezi kukiruhusu kwa sasa ni siasa za kizamani za kuwagawa watu, siasa ambazo tuliziona miaka ya nyuma iliyopita, yaani karne nyingi zilizopita,“amesema Barack Obama jana Alhamisi wakati akiwahutubia maelfu ya watu mjini Newark, New Jersey.

Obama akiwa jukwaani umati wa watu ulisikika ukitamka “Four more years” wakimaanisha aongeze miaka mingine 4 ya kugombea urais nchini humo.

Rais Obama aliendelea kurusha maneno bila kutaja waziwazi kuwa anamlenga nani huku akisikika akisema kuwa siasa za sasa anazoziona zilishapitwa na wakati, kwani hii ni karne ya 21 na sio karne 19.

Tunavyoona siasa za sasa, wengine wanadhani ndio tumefika, hizi ni siasa za miaka 50 iliyopita na hii ni karne ya 21, Kuna baadhi ya watu  wanajaribu kuwaudhi wenzao, kuwafanya wachukizwe na kuanza kuandamana kisa kupishana kimtazamo, muda mwingine mambo haya yanaudhi sana.“amesema Obama.

Kauli hiyo ya Obama imekuja saa moja baada ya Rais wa zamani wa taifa hilo, George Bush kutema cheche kwenye kampeni hizo akisema uongozi wa sasa uliyopo madarakani ni wa kuburuzana na wa chuki.

Hata hivyo, Marais wote hao hawajamtaja kabisa Rais Trump kwenye hotuba zao ingawaje wamelenga zaidi kuukosoa uongozi na hii inakuwa ni mara ya kwanza kwa marais wastaafu kuzungumzia utawala uliopo madarakani.

Uchaguzi wa Magavana nchini marekani unafanyika  tarehe 7 Novemba mwaka katika majimbo ya mawili tu ya New Jersey na Virginia na tayari wagombea wa Chama cha Democratic kwenye majimbo hayo wanapewa kipaumbele cha kuibuka washindi katika uchaguzi huo.

 

 

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents