Barakah The Prince awakata ngebe mashabiki wa Alikiba
Kwa muda mrefu sasa wadau wengi wa muziki wa Bongo Fleva wamekuwa wakiamini kuwa Msanii wa muziki wa Bongo Fleva, Barakah The Prince na mfalme wa Bongo Fleva, Alikiba wana bifu au tofauti miongoni mwao baada ya Baraka The Prince kujitoa kwenye lebo ya RockStar4000 ambayo ipo chini ya Alikiba na Meneja wake Seven Mosha.
Ukweli ni kwamba Barakah The Prince hana tofauti/bifu yoyote na Alikiba kama ambavyo mashabiki wengi wa Alikiba na wadau wa muziki walivyokuwa wakidhania kwani Hitmaker huyo wa Sometimes kupitia ukurasa wake wa Instagram amethibitisha hilo kwa kumtakia Kheri ya siku yake ya kuzaliwa Alikiba .
“Happy Birthday kaka King Kiba nakutakia maisha marefu“ameandika Barakah The Prince kwenye posti ambayo imeleta majibu kwa baadhi ya wadau waliokuwa wakidhani kuwa msanii huyo ana bifu na Alikiba.
https://www.instagram.com/p/BcFdhwigQWu/?taken-by=barakahtheprince_
Cheki maoni ya baadhi ya mashabiki wa Alikiba na wa muziki wa Bongo Fleva walivyotahamaki baada ya posti hiyo.
- franknenamye24 Ndo mashabiki wa mziki mzuri tunatakaga ivo ngosha bifu kwa wakongwe kama kiba haziwezi kukj
- taylor.gang.hookah Nyote ndugu Nyote Watanzania respect @barakahtheprince_ I salute u 💯 times fr this one
- kimatajr Ukiendelea hivyo hivyo #itapendeza_zaidi
- nurdinkhatib Hehehe unakaza wakikaza unajifanya fisi
- mrs_actorleeminho_koreanlove you more
- christianrangetz Mh ila ww dogo una mapepe mara umnifollow kiba mara umpost du
- hassanshaban218 Imependeza zaidi
- mrs_actorleeminho_korean@barakahtheprince ❤❤❤
- issa_smart@nurdin_product #baraka mbona hana tatizo na mtu huyu jamaa yuko poa sana ila watu wanashindwa kumuelewa tu.
SOMA NA HII – Alikiba anena Barakah kuondoka RockStar4000, ‘muache dunia imfunze’
Alikiba leo Novemba 29, 2017 anasherehekea siku yake ya kuzaliwa na mastaa kibao wamemposti kwenye kurasa zao za mitandao ya kijamii kumtakia maisha kheri akiwemo Ommy Dimpoz, Mwana FA, na wengineo.