Burudani

Barakah The Prince: Sitaki kumpa mtu ‘kiki’

Barakah The Price ameamua kujibu mapigo baada ya Bright kuongea kuwa hajui kuandika mistari na amekuwa akirudia rudia maneno katika nyimbo zake.

Akiongea kwenye E News ya EATV, Barakah amesema hawezi kuongelea lolote kuhusiana na hilo kwa kuwa hataki kuendelea kumpa kiki msanii mwenzake huyo ambaye alimshirikisha kwenye wimbo wa ‘Nitunzie’.

“Hiyo inaitwa unatafuta kiki kwa pikipiki, mimi siwezi kuongea nitakuwa nachafua brand yangu ya Rock Star na unajua mimi nikiongea watu wanazingatia sana, hivyo siwezi kuongelea watu kama hao katika interview zangu,” amesema msanii huyo.

Barakah ameongeza kwa kudai kuwa hamfahamu msanii anayeitwa Bright kwa kuwa anafanya kazi na wasanii wengi chipukizi.

Na Laila Sued

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents