Baraza la Wazee CHADEMA lataka kuonana na Rais Magufuli ‘Taifa limejaa uchungu’ (+video)

Baraza la Wazee CHADEMA Taifa, limeomba kukutana na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt John Pombe Magufuli kwa lengo la kujadili na kushauriana masuala mbali mbali yanayohusu Taifa letu ikiwemo masuala ya uchumi, usalama.

Roderick Lutembeka

Hayo yamesema leo Machi 13, 2018 na Katibu Mkuu wa Baraza la Wazee Chadema, Roderick Lutembeka kwenye mkutano wa Baraza hilo na Waandishi wa Habari.

Ndg. Roderick amesema taifa letu linapita katika kipindi kigumu na majaribu makubwa ya kisiasa, Kiuchumi na kijamii. Nchi inazidi kuvimba na watu wanahitaji kupumua hivyo kama taifa ni lazima lichukue hatua ya kusikilizana kati ya viongozi na wananchi. Tazama video hapa chini wazee hao wakiongea;

 

 

 

Related Articles

Bongo5

FREE
VIEW