Michezo

Barca vs Inter

Klabu ya Barcelona ya Hispania leo inawania kuingia Fainali katika mchezo wa pili wa marudiano wa kufuzu fainali katika mashindano ya klabu bingwa Ulaya yaani “Champions League”.

Barcelona ambayo pia inawania kuweka historia kwa kuwa timu ya kwanza kulichukua kombe hilo mara mbili mfululizo inapambana na kisiki cha Jose Morinho ambacho tayari kinanafasi ya kupita baada ya kuibuka na ushindi wa bao 3 -1 wiki iliyopita.

Mpambano huo ambao unasubiriwa kwa hamu na wapenzi wa Soka duniani kote unazikutanisha timu mbili zenye uzoefu wa hali ya juu katika mashindano hayo ambapo Barcelona inamtegemea zaidi lionel Messi wakati Inter Milan inamtegemea supa coach Morinho.

Tayari homa ya mchezo huo imeshapanda na wadau pamoja na mashabiki wanasubiri muda ufike ili waweze kuthibitisha kile kinachosubiriwa na wengi..Je Barca wataweza kupindua matokeo na kusonga fainali ama Inter itaweza kupigana kidete kuingia fainaliā€¦Jibu ni Rahisi Dakika 90 ama 120 ndio mwamuzi

Related Articles

Check Also
Close
Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents