Michezo

BARCELONA bingwa wa Ulaya

lionel_messi_fc_barcelona11

 Timu ya Barcelona ya Hispania imeendeleza ubingwa wake kwa mara ya nne katika ligi ya mabingwa wa Ulaya , kwa kuifunga Manchester United wa Englend kwa mabao 3-1  katika uwanja wa taifa wa Uingeleza  Wembley.


Bacerlona ilianzia kung’ara katika ligi yake ya ndani  baada ya kutwaa ubingwa wa lingi ya  Hispania maarufu kama La Liga chini ya uongozi wa Pep Guardiola, huku   wamepoteza mechi mbili tu.

Katika mechi ya leo, bao la kwanza lilifungwa mnamo dakika ya 28, lilikiingizwa nyavuni na Pedro ambalo liliwasha moto wa wachawi wekundu ama watoto wa Ferguson kuamsha moto.

Kama ilivyokawaida ya mabingwa hao wa Uingeleza walifanikiwa kurudisha goli hilo  kupitia kiungo wake mahili Wayne Looney katika  dakika ya 33.

Mpaka wanaenda mkekani kupumzika, mambo yalikuwa 1-1 huku wapenzi wakiwa hoi hai wakisubili dakika 45 za mwisho kujua hatma ya ligi hilo.

Waliporudi kutoka mapumziko ndipo, mambo hayakuwa mambo katika dakika ya 53, pale kijana  asiyetabirika na mwenye uchu wa magoli Leon Messe ulimshinda Van De San, na kuiandikia Bacerlona bao la pili, lakini hali ilikuwa mbaya katika dakika ya 70  David Villa aliposhindilia la tatu.

Mabao hayo yaliweza kuilaza Manchester, na kuipa ubingwa kwa mara ya nne timu ya  Barcelona .

Related Articles

Check Also
Close
Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents