Michezo

Barcelona: EPL ndo mpinzani mkuu kuliko Real Madrid

Rais wa klabu ya Barcelona Josep Maria Bartomeu amesema Ligi ya Uingereza ndo mpizani mkubwa wa Barcelona ikilinganishwa na Real Madrid.

maxresdefault

Ligi kuu ya Uingereza kuna Klabu 20 ambazo ndo zina shiriki zitaanza kugawanya kitita cha pauni bilioni 5.136 za matangazo ya moja kwa moja kuanzia msimu ujao.

”Timu za ligi ya Uingereza zitakuwa na ubabe wa kifedha kuanzia sasa na tuna wasiwasi,”Bartomeu aliiambia BBC Sports.

Kilabu ya Barcelona itapambana na Arsenal katika ligi ya vilabu bingwa Ulaya usiku wa Jumanne.

Kikosi cha Luis Enrique hakijafungwa katika mechi 32 za ligi na zile za kombe la ligi hiyo huku kikitaka kushinda kombe hilo kwa mara nyingine.

Kilabu kubwa za Uhispania -Barca na Real Madrid,zilijadili kuhusu mikataba yake ya mechi za ligi hiyo zinazoonyeshwa moja kwa moja katika runinga lakini sasa zimezuia kufanya hivyo kupitia sheria mpya ya Uhispania.

Source: BBC

Related Articles

Check Also
Close
Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents