Michezo

Barcelona kumfanya Dembele kuwa mchezaji ghali zaidi

Klabu ya Barcelona ya nchini Hispania wamepania kumfanya mchezaji wa Borussia Dortmund, Ousmane Dembele kuwa mchezaji ghali zaidi wapili baada ya Neymar kushika ya kwanza katika historia ya mchezo huo duniani.

Barca imeshamalizana na Dortmund kwa kutoa dau la Euro milioni 97 ili kumchukua mchezaji huyo kwa mkataba wa miaka mitano ambaye alikuwa miongoni mwa wachezaji wawili wanao hitajika kwa udi na uvumba akiwa pamoja na Philippe Coutinho wa Liverpool.

Dembele mwenye umri wa miaka 20 anatarajiwa kufanyiwa vipimo vya afya siku ya jumatatu na kukabidhiwa jezi namba 11 mgongoni.

Taarifa kutoka ndani ya Barcelona zinasema ,”FC Barcelona na Borussia Dortmund imeafikiana makubaliano ya uhamisho wa mchezaji Ousmane Dembele kwa dau la paund milioni 105 hii ikiwa nipamoja na mambomengineā€.

Kiasi hicho cha usajili kinafanya kuwa mchezaji wa pili ghali zaidi badala ya ya uhamisho uliyofanywa na PSG wadau la paundi milioni 200 kumsajili Neymar kutokea Barcelona.

Dembele raia wa Ufaransa alijiunga na timu hiyo ya Bundesliga kutoka klabu ya Rennes kwa Euro milioni 15 miezi 12 iliopita akiwa ameanza kucheza mwaka 2015.

By Hamza Fumo

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents