Burudani ya Michezo Live

Barcelona kumtimua kazi Ernesto Valverde muda wowote, Guardiola, Iniesta washindwa kuvumilia

Huwenda leo ikawa ndiyo siku ya mwisho kwa kocha Ernesto Valverde kuitumikia miamba ya soka nchini Hispania klabu ya Barcelona.

Image result for ernesto valverde

Licha ya Valverde kufika mazoezini mapema asubuhi ya leo kwa majira ya Hispania, lakini taarifa za kutimuliwa kwake kazi zimeenea baada ya viongozi wa ngazi za juu wa Barcelona kuitisha kikao cha kujadili hatma yake.

Rais wa Barcelona, Josep Maria Bartomeu na Wakurugenzi Javier Bordas, Oscar Grau na Eric Abidal walijifungia kwa saa kadhaa usiku wa jana siku ya Jumapili na kufanya mazungumzo ambayo yalimjadili hatma ya Valverde ambayo yamefanya kuibuka kwa taarifa kuwa huwenda akatimuliwa kazi leo siku ya Jumatatu.

Wakati Valverde akipitia kwenye kipindi kigumu baadhi ya mastaa ambao wamepitia Barcelona wamekuwa na maoni yao ambapo kocha wa zamani wa klabu hiyo na timu ya taifa ya Hispania, LuisEnrique amesema kuwa ”Valverde bado yupo kwenye nafasi yake ambayo anaweza kushinda mataji yote msimu huu.”

Huku Pep Guardiola akiongezea kuwa ”Najisikia vibaya kwake, hapaswi kwa hili,” wakati hayo yakiendelea fundi wa soka Andres Iniesta akiiambia Spanish radio Onda Cero kwamba “Njia ambayo klabu imekwendanayo juu ya jambo hili sio nzuri.”

Inadaiwa rais wa Barcelona, Bartomeu ni shabiki mkubwa wa Mauricio Pochettino na ndiye anayetarajiwa kuja kuchukua mikoba yake.

Related Articles

Back to top button
Close
Bongo5

FREE
VIEW