Burudani ya Michezo Live

Barcelona kuwapatia PSG nyota wake wawili tegemezi kwaajili ya Neymar, Messi ahusishwa kurudi kwa Mbrazil huyo

Klabu ya Barcelona na PSG zimekubaliana kuwatowa wachezaji wawili ili kubadilishana na mshambuliaji ghali zaidi kwa sasa duniani Neymar ili kujiunga na Wacatalan hao.

International Champions Cup El Clásico match FC Barcelona v Real Madrid

Barcelona ipo katika mipango ya kumrejesha Neymar kutoka PSG, hii ni baada ya miaka miwili tu kupita tangu kujiunga na matajiri hao wa Ufaransa akitokea Hispania.

Hapo jana siku ya Jumanne rasmi Mkurugenzi wa miamba hiyo ya soka kutoka Hispania alisafiri kuelekea Ufaransa kwaajili ya kufanya mazungumzo ya kumsajili nyota huyo raia wa Brazil.

Baada ya kutumia zaidi ya pauni Milioni 108 kumsajili Mfaransa, Antoine Griezman ilielezwa kuwa Barcelona ilikuwa na mpango wa kumchukua kwa mkopo Neymar ili kuepuka adhabu ya FIFA na hivyo kumsajili kwa dau kubwa msimu ujao.

Neymar

Lakini baada ya mazungumzo ya hapo jana baina ya viongozi wa timu hizo mbili imeripotiwa kukubaliana kwa kuwatoa wachezaji wawili ili kubadilishana na Neymar.

Kwa mujibu wa chombo cha habari nchini Hispania ‘Sport’ kimeripoti kuwa Barca watawtoa wachezaji wake wawili ambao n Philippe Coutinho na Ivan Rakitic ikiwa ni maombi ya PSG. Taarifa za ndani zinaeleza kuwa Lionel Messi ndiye aliyependekeza kurudishwa kwa Neymar.

Related Articles

Back to top button
Close
Bongo5

FREE
VIEW