Michezo

Barcelona wapatwa na pigo zito, Real Madrid ni shangwe tu kuelekea El Clásico

Klabu ya Barcelona jana usiku imeibuka na ushindi wa goli 4-2 dhidi ya Sevilla, ushindi ambao uligubikwa na simanzi baada ya mshambuliaji tegemezi wa klabu hiyo, Lionel Messi kuteguka kiwiko kunako kipindi cha kwanza cha mchezo huo.

Lionel Messi akiangukia mkono kwenye mchezo huo.

Messi ambaye alitupia goli moja na kutoa pasi moja ya mwisho (Assist) kwenye mchezo huo, atakuwa nje ya uwanja kwa wiki tatu jambo ambalo litamfanya akose mchezo wa Elclasico wikiendi ijayo.

Hii itakuwa ni mara ya kwanza kwa mchezo huo mkubwa duniani kwa ngazi za vilabu, Messi kutocheza tangu mwaka 2007.

Michezo mingine ambayo Messi hatacheza ni miwili ya Champions League dhidi ya Inter Milan, miwili ya La Liga na mmoja wa Kombe la Mfalme dhidi ya   Cultural Leonesa.

Hii itakuwa ni taarifa nzuri zaidi kwa mahasimu wao Real Madrid kuelekea El Clásico, kwani Messi ndiye mchezaji anayeongoza kufunga magoli mengi zaidi kwenye mchezo wa Elclasico katika historia amefunga magoli 26.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents