Soka saa 24!

Barcelona watoa sababu ya Kutumia lugha ya Kichina, kuandika majina ya wachezaji wao nyuma ya jezi katika mchezo wa #EL Classico leo

Klabu ya FC Barcelona imeamua kutumia lugh ya Kichina katika kuandika majina ya wachezaji wake nyuma ya jezi kwa lugha hiyo ya kichina.

Kupitia kurasa zake za mitandao ya Kijamii Brcelona wamesema:- “Katika mchezo wa El Classico leo dhidi ya Real Madrid wachezaji watavalia jezi zilizoandikwa majina yao kwa lugh ya Kichina ili kusherehekea mwaka mpya wa China kwa namna hiyo”

Ikumbukwe Jana tarehe 5/2/2019 ndio ilikuwa siku ya mwaka mpya wa Kichina ambao mwaka huo kwa wachina husherekea tofauti na mataifa mengi duniani ambayo husherehekea tarehe 1/1 ya kila mwaka, na Barcelona wameamua kuungana na Wachina kusherehekea sikukuu hiyo kwa namna ya kutumia Lugha yao kuandikia majina ya wachezaji wake ingawa Majina ya kawaida pia yatakuwepo.

By Ally Juma.

Related Articles

Back to top button
Bongo5

FREE
VIEW