Moto Hauzimwi
Shinda na SIM Account

Barkley atua Chelsea

Klabu ya soka ya Chelsea imekamilisha usajili wake wa kwanza katika dirisha hili kwa kunasa saini ya mchezaji Ross Barkley ambaye hapo awali alikuwa na klabu ya Everton.

Barkley amekuwa mchezaji ambaye amekuwa akiwindwa na klabu hiyo ya Chelsea kwa muda na hatimaye katua Stamford Bridge na atavaa jezi ya namba nane (8) ambayo ilishawahi kuvaliwa na nyota wa zamani wa klabu hiyo Frank Lampard na Oscar.

Muingereza huyo mwenye umri wa miaka 24 amenunuliwa kwa dau la pauni milioni 15 na ataitumikia klabu hiyo kwa muda wa miaka mitano na nusu.Barkley hajaonekana uwanjani kwa muda wa miezi saba tangu apate majeraha agosti 2017.

Meneja wa klabu hiyo ya Chelsea amesema kuwa mchezaji huyo ni mdogo na bado ana muda mwingi wa kuwa mchezaji bora.Pia aliongezea kwa kusema “He’s a good prospect but at the same time, it will be very important to understand, if the player signs,we must have patience to help him recover.”

Na Raheem Rajuu

Leave a comment

Related Articles

Bongo5

FREE
VIEW