Burudani

Barnaba amshauri Lulu haya kuhusu uigizaji wa filamu

Barnaba Elias ameusifia uigizaji wa Elizabeth Michael aka Lulu lakini amemtaka kubadilika na kutafuta aina moja ya uigizaji ambao utakuwa unamtambulisha.

Lulu michael

Akizungumza na kipindi cha DJ Show cha Radio One, Barnaba alisema anapenda kuangalia filamu za kibongo na anashangaa kuona watu wanabeza kazi hizo.

“Lulu anafanya vizuri lakini atambue anatakiwa kutafuta sehemu moja anayofiti, jinsi anavyokuwa mkubwa yanahitajika mabadiliko,” alisema.

“Mimi nashangaa watu wanaosema filamu za Bongo sio nzuri, mimi ni mpenzi mkubwa wa filamu za Bongo na sipendi kupitwa na movie yoyote. Hata nikisafiri kokote lazima niwe na filamu za kutosha za kuangalia, napenda sana za vichekesho na nyingine.”

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents