Burudani

Barnaba kuja na mradi uitwao ‘The Miracle Voice of Barnaba’

Msanii wa muziki toka THT, Barnaba Elias amesema anakuja na mradi alioupa jina ‘The Miracle Voice of Barnaba’ ambao utakuwa ni utaratibu wa kukaa na wasanii na wadau wa muziki na kujadili changamoto na kanuni za muziki.

barnaba

Akizungumza na 255 ya XXL ya Clouds FM leo,Barnaba amesema kuna wasanii wengi wanaofanya muziki lakini hawajui utaratibu na kanuni za muziki.

Nataka kufungua kipindi changu ambacho kitakuwa nimaweka kwenye website yangu ambacho kitakuwa kinaitwa The miracle voice of Barnaba,” alisema. “Sija plan vizuri kwasasa nipo kwenye project yangu nasimania ‘Jasho la Mnyonge’ kwahiyo video yangu na project zote zitakazoendelea kwenye ‘Jasho la Mnyonge’ na album yake nataka watu waanze kuviona kwenye barnaba.com. Nipo kwenye maandalizi ya The miracle voice of Barnaba ni maajabu ya sauti ya Barnaba kwa tafsiri ya Kiswahili. Ninachokifanya naalika watu wote ambao naamini kwa namna moja au nyingine hawajapata lile darasa la muziki kwenye kukaa kwa mazingira yenye mantiki ya muziki,” aliongeza.

“Kwahiyo kipaji nilichonacho na darasa nililonalo kupitia THT na uwezo wangu wa sauti na umahiri wangu wa muziki. Kuna wanamuziki ambao wamefanikiwa kwenye muziki lakini bado hawajui changamoto na kanuni za muziki, kwahiyo nitakachokuwa nakifanya kuwaalika watu kama itakuwa ni sebuleni au kwenye kochi langu nitawaita kwenye meza yangu ya The miracle voice of Barnaba na kufanya nao mahojiano na pia nitakuwa nafanya nao darasa la kuwahoji Je unafahamu key, je unafahamu mianguko, Je unafahamu wimbo wako uliimba kwa jinsi gani, kwa ajili ya kumpa darasa na afahamu ufunguo wake na muziki ni nini. Kwahiyo wale ambao wanaamini wanaimba vizuri lakini hawakupata darasa la muziki watapata na hata wanaokuja kwenye kuutengeneza muziki wa Tanzania ili wapate njia nzuri na kuipeperusha bendera ya Tanzania kupitia muziki.”

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents